19th Ave New York, NY 95822, USA

Ukweli kuhusiana na dawa ya Remdesivir

By Makinia Juma| August 23, 2021

Madai kwamba dawa ya Remdesivir ni aina ya chanjo iliyotengenezwa kufanyiwa majaribio barani Afrika si ya kweli. 

Kuanzia mwezi wa Septemba mwaka wa elfu mbili na ishirini watumizi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakisambaza picha za madawa yaliyo na maelezo, “Haifai kusambazwa Marekani, nchi ya Kanada na nchi zilizoko kwenye Umoja wa Uropa.”

Wengi wamedai kwamba maelezo yaliyo kwenye dawa hizo ni ushahidi tosha kuwa Nchi za Kaskazini mwa dunia zinatengeneza chanjo na kuzifanyia majaribio kwenye nchi zisizojiweza. 

Picha hii ilianza kusambazwa katika mitandao ya kijamii kwenye nchi kadhaa barani Afrika. “Amkeni Afrika, huu ni mtego na wala sio dawa za kuponya ni jama ya kuwatumia kama panya wa majaribio katika maabara.” Jumbe moja ilisema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mwezi wa Septemba mwaka uliopita. 

Mwezi wa Januari mwaka huu, picha za aina aina zilizotokana na Picha hii zilizuka tena kwenye mtandoa wa kijamii wa Facebook. 

Posti moja kwenye mtandao wa Facebook hapa nchini Kenya iliuliza wataalam wa ugonjwa wa Covid-19 ni kwa nini chanjo hiyo ifanye kazi kwenye nchi za Afrika pekee, posti hii ikiongezea kwamba, “Ugonjwa unaoathiri bara la Afrika, Umoja wa Uropa, nchi ya Kanada na Marekani ni ule ule mmoja wa Covid-19.”

Posti hii ilikuwa na picha mbili za madawa.  Picha ya kwanza ilionyesha sehemu ya mbele ya boxi la dawa ya Remdesivir ikiwa imeandikwa, “Sindano ya Remdesivir miligramu 100 kwa konteina moja,” ikifuatiwa na taarifa, “Haipaswi kusambazwa nchi ya Marekani, Kanada na Umoja wa Uropa.”

Kwenye sehemu ya nyuma ya boxi lenye dawa hii kuna taarifa, “Kwa matumizi katika nchi zilizo orodeshwa hapa peke yake.” Nchi hizi zikiwa nchi harubaini na saba za Afrika. 

Posti iliyoweka picha hii imesambazwa kwa makundi mengi mtandaoni na imepata majibu na jumbe nyingi tangu ilipowekwa mtandaoni mwezi wa Septemba. 

Lakini je, madai kuwa chanjo ya Remdesivir ni chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 na kwamba inafanyiwa majaribio barani Afrika ni ya kweli…?

 

Si Chanjo

Shirika la Afya la Dunia linasema, chanjo; inasisimua mwili ili kusababisha kinga mwilini dhidi ya wadudu na virusi vinavyosababisha ugonjwa huu. 

Remdesivir si chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, ni dawa ya kupigana na virusi iliyotengenezwa kupigana na kutibu virusi mbali mbali. Covifor ilionyeshwa kwenye picha ya kwanza ni aina inayohusika na dawa ya Remdesivir. 

Kulingana na huduma ya Afya ya Hetero, Covifor ni sindano ya kutibu wagonjwa wa Covid-19 walio na dalili kali za ugonjwa huo na wala si chanjo. 

Kwa kauli iliyotolewa tarehe ishirini na nne mwezi wa Juni mwaka wa elfu mbili na ishirini , Kampuni yenye kutengeneza dawa ya Covifor ilisema kwa kupitia kwa dawa hii wanatumahi kupunguza wakati wa kutibiwa kwa wagonjwa wenye Covid-19 hosipitalini, huku wakiongeza kuwa watapunguza shinikizo kwa huduma za kimatibabu amabazo ziko na upungufu wakati wa janga hili, visa vinapozidi kuongezeka. 

Kampuni hiyo ya kutengeneza madawa iliendelea kusema, “Covifor ni aina ya kwanza inayohusika na dawa ya Remdesivir ikiwa ya matumizi ya kimatibabu kwa watu wazima na kwa watoto waliolazwa na dalili kali za ugonjwa wa Covid-19.”

Watafiti walifanya majaribio na kupata kuwa dawa hii imeonyesha ufanisi kwa virusi vya Corona kama MERS na SARS. 

FDA ilipeana idhini ya dharura mwezi wa Oktoba mwaka wa elfu mbili na ishirni kwa dawa ya Remdesivir kutumika kwa visa vibaya zaidi vya Covid-19. Dawa hii ikionekana kwenye majaribio ya kliniki kupunguza muda wa kupata nafuu kwa wagonjwa kadhaa wa Covid-19. 

Mwezi wa Novemba mwaka wa elfu mbili na ishirini Shirika la Afya la Dunia, shirika linalohusika na afya ya uma la ndani ya nchi, ilitoa masharti ya kimaelezo, ikisema, Remdesivir isitumiwe kwa wagonjwa wa Covid-19 waliolazwa. 

Shirika hilo likiongeza, “Kwa sasa hakuna ushahidi kuwa Remdesivir inaimarisha hali au kupona haraka kwa waathiriwa wa ugonjwa wa Covid-19.”

Tarehe 12 mwezi wa Februari mwaka wa elfu mbili na ishirini na moja, Kituo cha kudhibiti magonjwa kilichapisha miongozo na maelezo kulingana na ushahidi wa kisayansi, ya usimamizi na matibabu ya waathirwa wa SARS-CoV-2, kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Covid-19. 

 

Kupewa leseni ya usambazaji duniani. 

Tovuti ya Gilead inaeleza makubaliano ya kileseni yanaruhusu watengenezaji kutengeneza dawa ya Remdesivir kwa usambazaji kwa nchi mia moja ishirini na saba zenye viwango vya kati kati na vya chini vya maisha duniani. 

Vile vile kuna orodha ya nchi hizo kwenye tovuti yao, orodha hiyo ni pamoja na nchi harubaini na saba zilizo orodheshwa kwenye picha iliyosabazwa kwenye mtandao wa kijamii na madai ya mtego, pamoja na nchi kutoka bara la Marekani Kusini, Uropa na Asia. 

Nchi ya Kanada, Marekani na nchi zilizoko katika Umoja wa Uropa hazipo kwenye orodha hiyo lakini hii haimaanishi kwamba kampuni ya Gilead haisambazi dawa hizo kataki nchi hizo. 

Mwezi wa Agosti mwaka wa elfu mbili na ishirini nchi ya Kanada ilipeana idhini ya matumizi ya dawa hii na hivyo basi kuiweka kwenye mfumo wake wa afya kwa uma. 

Kampuni hii ya madawa mwezi wa Oktoba mwaka wa elfu mbili na ishirini, ilitia sahihi makubaliano ya muungano wa ununuzi na tume ya Uropa kusambaza dawa hii katika nchi za Umoja wa Uropa. 

Tukitumia ushahidi niliyoupeana hapo awali, madai kwamba dawa ya kupigana na virusi ya Remdesivir ilitengenezwa na itafanyiwa majaribio barani Afrika si ya kweli. 

This is an edited and translated version of a story by Makinia Juma which originally appeared on Khusoko.