19th Ave New York, NY 95822, USA

Ufuatiliaji wa janga kubwa kwenye mitandao ya kijamii

By Ireri Brian Murimi| August 23, 2021

Maelezo ya Muhariri

Mtaalam wa virolojia mwenye utata Luc Montagnier kutoka nchi ya Ufaransa hakusema kuwa watu wenye kupashwa chanjo watakufa katika muda wa miaka miwili. Hii ni habari njema kwani katika nchi zingine kama Uingereza takriban asilimia tisaini ya watu wazima wameshadungwa sindano. Ulimwenguni, kama ujumbe unaosemekana kuwa wa Bwana Montagnier ungekuwa wa kweli ungemaanisha vifo vya mabilioni ya watu.

Moja wapo ya njia rahisi za kuweka ujumbe wa uwongo kwenye video ni kwa kubadilisha sauti. Na moja wapo ya njia za kuhakikisha kutokujulikana kwa ujumbe wa uwongo ni kwa kuweka sauti kwa lugha inayohitaji kutafsiriwa, hii inaeleza kwa nini orodha ya sauti ya awali haiwezi kuwa kwenye video hiyo. Vile vile njia nyingine yakueneza habari za uwongo kwenye video ni kwa kuweka maandishi ya kutafsiri kwenye video hiyo. 

“Watu wote waliopashwa chanjo watakufa kwa muda wa miaka miwili.”

Huu ulikuwa mwanzo wa ujumbe uliosambazwa kwa wingi kwenye mtandao wa Whatsapp ukimwonyesha mshindi wa tuzo la Nobel na Mtaalam wa virolojia Luc Montagnier akidai kuwa hakuna kupona kwa yooyote aliyepashwa chanjo dhidi ya maradhi ya Corona. 

“Hakuna tumaini wala matibabu yanayoweza kuwasaidia wale ambao wameshapashwa chanjo. Tujitayarishe kuchoma miili.”

Lakini madai haya yanayosemekana kuwa ya Bwana Montagnier ambaye amewasilisha jumbe za kukataa kupashwa chanjo hapo awali, si ya kweli. Na wala hayana kuungwa mkono na data yoyote ya Kisayansi. 

Citizens who have taken the Vaccine
Citizens who have taken the Vaccine

 

Habari hizi potovu ambazo husemekana kuwa za watu wenye umaarufu ili kusaidia kuaminika kwake, zimejaa kwenye mtandao na kuregesha nyuma vita vya kuangamiza janga la Corona. 

Madai haya ya uwongo na ya kupotosha yamesambazwa nchini kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Whatsapp. 

Hata kabla ya watu wenye mamlaka kutangaza kuwepo kwa kisa cha kwanza cha Ugonjwa wa Covid-19 takriban mwaka mmoja uliopita, picha na video zenye habari potovu kuhusiana na Ugonjwa huu zilikuwa zishasambazwa. 

Kutokuwepo kwa bidhaa madukani, foleni ndefu za watu madukani na picha za tishu zilizonunuliwa kwa wingi zilikuwa mojawapo ya picha na video zilizojaa kwenye mitandao.

Kati kati ya mwezi wa Machi mwaka wa elfu mbili na ishirini idadi kubwa ya watu walijaa kwenye maduka ya kununua bidhaa ili kununua vitu kwa wingi kabla ya karantini. Huku wengi wakinunua bidhaa za muhimu za kujikimu kimaisha. 

Kenyans line up at Quickmart supermarket in Nairobi a day after the first coronavirus case was announced in the country. Photo: Crime_KE/Twitter
Kenyans line up at Quickmart supermarket in Nairobi a day after the first coronavirus case was announced in the country. Photo: Crime_KE/Twitter

 

Wingi wa habari potovu kuliwafanya Waangalia ukweli kukaa makini. 

Africa Check, shirika lisilo la kiserikali la kuangalia ukweli, iliweka muongozo wa wazi wa ugonjwa wa Corona kuanzia mwanzo wa janga hili na imetupilia mbali mengi ya madai haya ya uwongo. 

Kulingana na shirika la Africa Check habari potovu humu nchini zimesambaa kwa njia kadha wa kadha kama maudhui ya uwongo, kutapeliwa kwa jumbe, madai yenye upotovu na ya uwongo. 

Screengrabs of some of the misinformation and disinformation that had a great impact in Kenya.
Screengrabs of some of the misinformation and disinformation that had a great impact in Kenya.

 

Kutupilia mbali madai ya uwongo. 

Moja wapo ya madai haya hivi karibuni yalitoka kwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya Bi. Mercy Mwangangi aliyesema nchi ya Kenya ni nambari saba katika zoezi la usambazaji wa chanjo. 

“Kwa sasa tuko nambari saba kwenye msururu wa wanaoongoza na tuko na mipangilio ya kupanda kwenye nafasi ya juu zaidi,” Bi Mwangangi alisema akiwahutubia wanahabari. 

Huu ni uwongo. Data iliyotolewa inaonyesha kuwa nchi ya Kenya ikiwa mbele ya jirani zake Mashariki ya Afrika, imepeana chanjo kwa asilimia mbili tu ya wananchi. 

Video hii ya madai ya kupotosha kufikia sasa imeangaliwa na watu elfu mia moja sitini na mbili tangu wakati wa kuchapishwa kwake kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook. 

Video hiii iliposambazwa, Kenya ilikuwa imepeana chanjo kwa idadi ya moja nukta tatu kati ya watu mia moja dhidi ya wastani ya ishirini na tatu kati ya watu mia moja inayotakiwa duniani. Kufikia tarehe ishirini na nne mwaka wa elfu mbili ishirini na moja nchi zinazoongoza zoezi la upashaji chanjo zilikuwa zimepasha chanjo watu harubaini na saba na mia moja na ishirini na moja kati ya watu mia moja hii ni kulingana na data ya Dunia inayofuatilia ugonjwa wa Corona. 

Kulingana na Daktari Subiri Obwogo mshauri wa kutia nguvu mifumo na sera za afya, mitazamo ya viongozi ni ya muhimu wakati wa Janga lolote. 

“Kuwa na mfumo wa sawa wa kiafya na mitazamo ya kufaa ya viongozi ni mambo ya muhimu nchi inapokabiliana na janga. Kama tunavyopenda kusema manufaa ya habari njema si ufuhamu bali ni matendo.” Daktari Obwogo alisema. Daktari huyu ni moja wapo ya wanaokaa kwenye kundi la serikali kutoa ushauri ya jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. 

Habari potovu zimewaweka wengi hofu badala ya kuwatia moyo kupitia kwa miongozo ya sawa ya kiafya. Baada ya kisa cha kwanza kutangazwa nchini, picha iliyojuu ya majeneza yakiwa na maua ilisambazwa na kuangaliwa sana kwenye mtandao. 

Picha hii inayodaiwa kupigwa nchini Italia iliwaonya wakenya kujitahidi iliwasipatwe na hali kama hii. 

Uchunguzi wa picha kupitia chombo cha mtandao cha TinyEye unaonyesha picha hii ilichukuliwa tarehe ishirini na nane mwezi wa Septemba mwaka wa elfu mbili na kumi na tano. Picha hii ilichukuliwa na mpiga picha wa AFP Alberto Pizzoli inaonyesha majeneza yaliyopangwa katika uwanja wa ndege wa Lampedusa na ni ya waathiriwa wa kuzama kwa dau lililokuwa limebeba wahamiaji na kuwauwa mamia ya watu. 

A screengrab of a Google Reverse Search of an image widely spread in Kenya to depict deaths caused by COVID-19 in Italy.
A screengrab of a Google Reverse Search of an image widely spread in Kenya to depict deaths caused by COVID-19 in Italy.

 

Janga la Corona linapofikia mwaka wake wa pili, wengi wamezoea kupata takwimu kuhusiana na ugonjwa huu. Uchunguzi kwenye mitandao unaonyesha kuwa watu bado wanatafuta habari kwa wingi kwenye mitandao kumaanisha kuwa shida ya habari potovu kuhusiana na ugonjwa huu bado itaendelea. 

This is an edited and translated version of a story by Ireri Brian Murimi which originally appeared on Tv47