19th Ave New York, NY 95822, USA

Nilikunywa chai ya chumvi kukinga ugonjwa wa Corona/ COVID-19

By Tabitha Otieno| August 23, 2021

Maelezo ya Mhariri

Siku za awali za janga la Corona, ni machache yaliyokuwa yakijulikana kuhusu ugonjwa huu. Uvumi ulikuwa mwingi na bila dalili ya tiba, jumbe za uwongo zisizo na msingi zilianza kuenezwa kwa wingi; na haikuwa na watu washirikina pekee. Watu waliosoma na wenye ujuzi, hata ujuzi wa kimatibabu walieneza uvumi bila ya kudiriki ukweli wake au chanzo cha jumbe walizokuwa wakieneza. UJumbe kuwa maji moto au maji ya chumvi yanaweza kukinga ugonjwa huu ulienezwa ulimwenguni kote.  Kati kati ya mwezi wa Machi mwaka wa elfu mbili na ishirini jumbe moja kwenye mtandao ikidai kuwa madaktari nchini Japan wanashauri watu wasukutuwe na maji ya chumvi ulienezwa kwa wingi huku ukweli wake ukitupiliwa mbali. Ujumbe huu bado upo na unaenezwa hadi hii leo. 

“Nilikunywa chai ya rangi na chumvi ili kukinga ugonjwa wa Covid-19,” mwanahabari nchini Kenya anajuta. 

Eneo la Tana River, Kenya: Busara Naaman alikuwa amelala wakati kubishwa kwa mlango wa chumba chake saa tisa za asubuhi, kulimuamsha. 

Yaya wa mtoto wake alikuwa amesimama mlangoni, simu mkononi akimwambia yuko na habari za dharura za kumueleza. Wazazi wake walikuwa wamempigia simu saa nane za usiku kumwambia kuwa kuna uwezekano kumepatikana tiba ya ugonjwa wa Covid-19. 

Yaya huyu hakuwa na wakati wa kupoteza kwa hivyo alimuamsha Mkubwa wake. 

“Nilikunywa chai na chumvi na wala si sukari. Ilikuwa na majani mengi ya chai na chumvi ilitupate kinga kutokana na maradhi ya Corona,” Naaman anaeleza. 

Kulingana na habari kutoka kijijini, mtoto alizaliwa na mtoto huyo alizungumza kwa sekunde kadha. Aliwaeleza watu wanywe chai na chumvi masaa ya mapema kama saa tisa za asubuhi hivi ilikupata kinga kutokana na ugonjwa wa Corona. Kwa hivyo, hivyo ndivyo tulifanya,” anatuelelza. 

Busara Naaman
Busara Naaman

 

Kijiji anachoishi Naaman kiko katika kaunti ya Tana River mkoa wa pwani ya Kenya. Mtu ambaye anamuamini na alitumahi angemuhakikishia ujumbe huu ni baba yake mzazi. Sababu ikiwa anaishi sehemu hiyo na ujumbe kuhusiana na chai ya chumvi ulitoka kwake kwani wana uhusiano wa karibu wa baba na mtoto wake wa kike. 

“Nilimpigia simu baba yangu saa tisa za asubuhi na kumuuliza, umepata habari…? Akaniambia ndio. Nikamuuliza tufanyeje…?” Anasema Naaman akinakili mazungumzo yake na baba yake. 

“Alinieleza ni vizuri kufanya vile watu wanavyofanya sababu ikiwa inaweza kuwa nyakati za mwisho na watu wanaelekea mbinguni alafu wewe ukose kwenda. Ina maana kwamba utaachwa nyuma, usikubali kuachwa nyuma,” anaeleza Naaman. 

“Namuheshimu baba yangu sana. Mimi humuomba ushauri kwa jambo lolote kwa hivyo alivyonieleza ninywe, nilikunywa,” Naaman anaeleza. 

Naaman anasema alimuamsha mtoto wake mchanga wa miezi minane aliyekuwa amelala na akamwangalia akinywa kinywaji hiki kwa shida.

“Mtoto wangu alikuwa mchanga ilinipa uchungu kumwona akinywa kinyaji hicho, “anasema. 

Wakati huo elimu madarasani ilikuwa imekatizwa nchini Kenya kuzuia uenezi wa ugonjwa wa Corona. Mmoja wa wanafunzi aliyepokea simu kutoka kwa mtu wa jamii yake aliusambaza ujumbe huo kwa wazazi wake. 

Hahoya Nuru ambaye pia ni mkaazi wa kaunti ya Tana River anaeleza pia yeye alikunywa kinywaji hiki cha miujiza. 

“Mtoto wangu wa kike alikuja na habari akinambia amepokea simu kwamba kabla ya saa sita usiku kila mtu anafaa awe amepika chai na kunywa ili kujikinga kutokana na ugonjwa wa Corona. Kwa sababu ya hofu na wasiwasi na vile habari kuhusiana na janga hili zilikuwa za kutisha hatukuwa na budi bali kunywa kinywaji hicho, “ anaeleza Hahoya.

 

Hayo Nuru
Hayo Nuru

 

Hahoya wa miaka thelathini na tisa ambaye hatumii majani ya chai kwa sababu za kiafya, anaeleza vile ambavyo alibidi aende hospitali kwa sababu ya madhara aliyoyapata kutokana na kunywa chai hiyo. 

“Ni afadhali nipashwe chanjo kuliko ninywe chai ya majani chai au kufanya chochote kingine ambacho hakijahakikishwa na madaktari kitakacho nidhuru. Nakumbuka nilipokunywa chai ya majani chai ilinibidi niende hospitali kwa sababu ya shida niliyo nayo ya vidonda vya tumbo,” anasema Hahoya. 

Ujumbe kuhusu chai hii ya rangi ulikuwa kanda ya sauti. Ilisambazwa kwa wingi kwenye mtandao wa Whatsapp. Walioupokea ujumbe huu waliusambaza kwa watu wa jamii zao na kupigiana simu usiku huo huo. Hata kama Busara Naaman alipata ujumbe wa kwanza kutoka kwa Yaya wa mtoto wake anakumbuka kuupata ujumbe huo huo baadaye kwenye mtandao wake wa Whatsapp. Hakumbuki mweye kumtumia au vile alivyoupoteza ujumbe huo kwani alinunua simu mpya. 

“Ilikaa kama mambo ya uchawi kwani wanadai kuwa mtoto aliyezaliwa Tana River alizungumza kwa madakika kadhaa kisha akafa. Nilitaka kuhakikisha hili kwani lilikaa jambo lisilo la kawaida lakini kila mtu aliliamini. Hadi baba yangu mzazi alikunywa chai hii ya rangi na jambo la kuchekesha ni kuwa tuko na kundi la kifamilia kwenye mtandao wa Whatsapp, kila mtu kwenye familia yetu alikunywa chai ya chumvi,” anasema Naaman.

Akiangalia nyuma anasema anajilaumu yeye binafsi kama mwanamke aliyesoma kwakuanguka mtegoni ili asiachwe nyuma. 

“Ni kinaya kwani mimi ndiye mwanahabari, nafaa niwe na ukweli. Nafikiri nilikuwa nimechanganyikiwa, lilikuwa jambo la haraka na ilikuwa masaa ya kuchelewa ya usiku na kila mtu alikuwa anakunywa. Jambo ambalo halikuwa la kawaida ni kwamba mimi, mtu aliyepaswa kuwa na habari na ufahamu sikuwa nao,” anasema Naaman. 

Busara anasema kuwa hakuna aliyekunywa chai hiyo ya chumvi kutoka kwa familia yake aliyekuwa mgonjwa au kufa. Anashukuru kwamba haikuwa sumu.

“Sisi hunywa chai kwa sukari lakini awamu hii ilikuwa tofauti. Ilionja vibaya kwani chumvi ni ya mchuzi au kachumbari na wala si ya chai. Niliweza kunywa kikombe nusu peke yake,” anasema. 

Siwezi fanya jambo kama hilo tena, hivi sasa najua vyema zaidi, naelewa ugonjwa wa Corona vyema. Kama majuzi mtu alituma ujumbe uliokuwa na habari potovu kuhusu ugonjwa wa Covid-19 kwenye kundi la mtandao la Whatsapp. Niliamua kuhakikisha habari iliyokuwa kwa ujumbe huo na Mhariri wangu na tukapata kuwa ujumbe huo ulitoka kwenye tovuti ya uwongo,’’ anamalizia. 

Mkurupuko wa ugonjwa wa Covid-19 umefwatiwa na muongezeko wa habari potovu. Muongezeko huu ukiwa tangu mwanzo wa ugonjwa huu, mwezi wa Machi mwaka wa elfu mbili na ishirini, kwenye mitandao ya kijamii ambapo jumbe hizi zilikuwa zikienezwa kukasababisha uenezi mwingi wa habari za uwongo kama vile uvumi kuhusiana na chai ya rangi. 

Kutafuta kwenye mtandao wa Google kunaonyesha matokeo mengi kuhusiana na chai ya rangi. Moja wapo ikiwa ni video kwenye mtandao wa YouTube kutoka kwa muumini wa kiume wa dini ya kiislamu akiwasihi waisilamu wenzake wasiwe waathiriwa wa habari potovu bali wamuombe Mungu wao. Ujumbe huu umerekodiwa kwenye lugha ya Kiswahili inayozungumzwa sana mkoa wa Pwani ya Kenya. Video hii ilichapishwa tarehe ishirni na tisa mwaka wa elfu mbili na ishirini na imeangaliwa na watu zaidi ya elfu sita. Mzungumzaji kwenye video hiyo anasema picha na video kuhusu chai ya rangi zilisambazwa usiku uliopita kabla ya kurekodiwa kwa ujumbe wake na anasema kuwa ujumbe huo wa chai ya chumvi ni wa uwongo. 

Kutafuta kwenye mtandao wa Facebook vile vile kunaonyesha ujumbe wa Katibu mkuu wa mawasiliano ya Ulimwengu wa Umoja wa Mataifa Melissa Fleming. Tarehe ishirni na tisa mwaka wa elfu mbili na ishirini, ujumbe wake ulieleza wasiwasi kwa muongezeko wa kuenea kwa habari zinazo potosha kuhusiana na ugonjwa wa Covid-19. Alisema ili watu kuangamiza ugonjwa wa Corona, kuna uhitaji kwa watu kupeana kipaumbele kwa ukweli, sayansi, tumaini na umoja na wala sio kufa moyo au utengano. 

“Timu yangu ya ulimwengu katika Umoja wa Mataifa itaongeza jitihada za mawasiliano yetu kuhakikisha watu wamepata habari za kweli na zilizo bora zaidi. Vile vile na mifano yenye kutia moyo na matendo ya kibinadamu,” hii ikiwa sehemu ya posti aliyoweka Bi. Flemming. 

Kwenye mtandao wa Twitter habari hii ilifanywa na vyombo vya habari vya NTV ambapo wataalam walidhihirisha kuwa chai ya chumvi si tiba ya ugonjwa wa Covid-19.

Twitter Post on Black Tea and Covid-19
Twitter Post on Black Tea and Covid-19

 

This is an edited and translated version of a story by Tabitha Otieno which originally appeared on Talk Africa.