19th Ave New York, NY 95822, USA

Mazingira magumu, Unyanyapaa na habari potovu kuhusu ugonjwa wa Covid-19

By Sigomba Ramadhan Omar| August 23, 2021

Maelezo ya Mhariri

Tangu kuchipuka kwa mtandao kutapeliwa au kupotoshwa kupitia kwa kuchanganywa kwa picha ili kupeana ujumbe wa kupotosha ni moja wapo wa njia maarufu zinazotumika kulaghai watu. Picha nyingi zilizoenezwa za watu kufa kwa ugonjwa wa Corona zilikuwa picha za kale. Si kawaida na haiwezekani kwa watu kuacha miili ya wafu barabarani. Mara nyingine haijulikani kwa nini au kwa sababu gani picha hizi huchanganywa lakini mwishowe shughuli hii huleta kutokuamini. 

“Habari za uwongo zingeniuwa kabla ya virusi vya Corona,” ananieleza Kibet Rono muathiriwa wa ugonjwa wa Covid-19 anaponieleza safari yake ya kupata afueni.

Mkulima huyu wa miaka hamsini na sita anayefanya kazi eneo la Kesses kaunti ya Uasin Ngishu ni moja wa wakenya wengi aliyeamini habari za uwongo na kujawa na hofu na kukosa tumaini. 

Huku akitabasamu ananieleza alikuwa kati ya wakenya wengi waliokimbia madukani kununua bidhaa za matumizi kwa wingi kutokana na hofu baada ya kisa cha kwanza cha Corona kuripotiwa  mwezi wa Machi mwaka wa elfu mbili na ishirini.

Rono ambaye pia ana ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu anakumbuka jinsi alivyokuwa na hofu aliposikia ripoti kwamba watu Italia walikuwa wakifa kwa maelfu. 

One of the images Rono came across falsely claiming that people were dying in the streets of China. [Courtesy]
One of the images Rono came across falsely claiming that people were dying in the streets of China. [Courtesy]

Rono ambaye alitembelea nchi ya Italia mwaka wa elfu mbili na kumi na tisa aliigia wasiwasi kuwa angefariki kama wengi waliofariki Italia kutokana na ugonjwa huu. 

“Nilitamani kukimbia. Najua wengi walihisi hivi. Kulikuwa na hali ya sintofahamu. Hakuna aliyejua kilichokuwa chaja. Kusema ukweli nilikuwa na hofu, haswa kwa sababu nilikuwa Italia kabla ya mkurupuko wa ugonjwa huu,”ananieleza. 

Bwana Rono alipata ugonjwa huu mwezi wa Juli 2020.

“Nilikuwa mgonjwa na kulazwa hosipitali kwa wiki tatu. Ilikuwa kama kuwa na mchangayiko wa ugonjwa wa malaria na homa ya matumbo.”

Akikumbuka picha za uwongo za miili ya watu waliokufa ikiwa imetandazwa katika nchi ya Uchina na picha za majeneza  ya waathiriwa wa Covid-19 Italia, Rono anasema alifanyiwa unyanyapaa alipoambukizwa ugonjwa wa Covid-19. 

“Nilikuwa karibu kupoteza tumaini, niliogopa sana.”

Baada ya wiki tatu za matibabu, Rono alisikia nafuu. Anasema Madaktari walimpa dawa za kumsaidia kupumua. 

Kufuatilia Picha. 

Utafiti kupitia kwa chombo cha mtandao cha Yandex kilionyesha kuwa picha ya miili ya watu waliokufa kwa ugonjwa wa Corona Uchina ilichukuliwa na mwanahabari wa vyombo vya habari vya Reuters, Kai Pfaffenbach tarehe ishirni na nne mwaka wa elfu mbili na kumi na nne nchini Ujerumani. 

Picha hiyo ilikuwa imeandikwa, “Watu walala barabarani kuwakumbuka waathiriwa mia tano ishirini na nane wa kambi ya ukolezi wa Katzbach wajerumani. 

Hapa Kenya picha hii iliwekwa na mtumizi kwa jina la Barakallahu Feek tarehe ishirini na saba mwezi wa Januari mwaka wa elfu mbili na ishirini, saa nne na dakika harubaini na sita ikisema kuwa watu wanakufa mabarabarani Uchina. Kufikia kuchapishwa kwa makala haya picha hii ilikuwa imeshasabazwa kwa watu harubaini na tisa na kutumwa kwa watu themanini na moja na kupata jumbe sitini na saba kutoka kwa watu wasiokuwa na ufahamu wa chanzo chake. 

Some of the photos shared online falsely depicting Covid-19’s dreadful impact. [Courtesy]
Some of the photos shared online falsely depicting Covid-19’s dreadful impact. [Courtesy]

Picha nyingine ambayo Rono aliiona ilikuwa mkusanyiko wa picha nne ikionyesha mkusanyiko wa majeneza mengi  na ujumbe unaosema, “Hali ilivyo Italia.” Ujumbe huu ukionyesha kuwa ugonjwa wa Covid-19 umewauwa wengi katika bara la Uropa. 

Uchunguzi kupitia kwa Chombo cha utafiti cha Yandex kinaonyesha kuwa picha hii ya majenenza ilichukuliwa Italia. Lakini haikuwa ya waathiriwa wa Covid-19. 

Nilipata moja wapo ya picha hizo kwa tovuti ya AFP. Kulingana na AFP picha hii ilipigwa Italia Kusini mwezi wa Oktoba mwaka wa elfu mbili kumi na tatu wakati dau lilipopenduka na kuzama na kuwauwa mamia ya wahamiaji. 

Nilipotumia TinyEye chombo kingine cha uchunguzi nilipata picha nyingine kati ya nne zilizochanganywa ya wanawake wawili waliopiga magoti kando ya jeneza lililoko na maua kuwa habari ya Kituo cha habari cha Los Angeles Times kuhusiana na mtetemeko wa arthi Italia mwaka wa elfu mbili na tisa. 

Baada ya uchunguzi wa muda mtandaoni nilipata moja wapo ya picha kwenye mtandao wa kijamii kwenye ujumbe wa Twitter, mtumizi kwa jina la Jeff M, amabyo ilifanana na picha aliyoiona Rono. 

Rono ni mmoja wa walioathirika na habari potovu. Lydia Chepkurui muuzaji wa nguo za mitumba, bado hajapata nafuu baada ya kuamini habari potovu kuwa serikali itakataza uagizaji wa nguo za mitumba nchini kwa miezi miwili. 

“Kama mwanabishara mwengine, biashara yangu ilipata changamoto. Mpaka sasa bado haijarejea kawaida kwani faida bado iko chini tangu kukatazwa kwa uagizaji,” anatueleza.

Chepkurui anasema kuwa kulikuwa na dalili nzuri mwanzoni mwa mwaka, lakini baada ya vikwazo vilivyowekwa hivi majuzi hatujui kama hali itaimarika. 

Serikali ilikataza uagizaji huu kwa madai kuwa ungesaidia kueneza ugonjwa wa Corona. 

Corona sio mwisho wa maisha. 

Kulingana na data kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins, Idadi kamili ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ulimwenguni kwa kufikia kuchapishwa kwa makala haya ni milioni mia moja sitini na tisa, huku maafa yakifika milioni tatu nukta tano. Nambari hii ikitarajiwa kuongezeka. 

Hapa Kenya maambukizi yamefikia zaidi ya visa elfu mia moja na sabini, watu elfu mia moja na kumi na sita wakipata nafuu. Zaidi ya vifo elfu tatu vimeripotiwa lakini nambari hii inashukiwa kuwa juu zaidi kwa sababu ya ukosefu wa vipimo. 

Kulingana na data kwenye Shirika la Afya la Dunia, vifo kutokana na ugonjwa wa Corona nchini Kenya viko na uwiano wa asilimia moja nukta nane. 

Saikolojia ya habari za uwongo

Mitandao ya kijamii imezidisha kuenea kwa habari potovu kwa kuwapa waenezi wa habari za uwongo sehemu huru za watumizi wa mtandao kuweka habari na ripoti za kusisimua

Umoja wa Kimataifa ulitoa onyo kuhusiana na athari za kisaikolojia za kusambaza habari za uwongo na potovu kuhusiana na maradhi ya Corona. 

Alphonse Shiundu kiongozi wa kuangalia Ukweli nchini Kutoka Kituo cha Kuangalia Ukweli cha Afrika, anasema wasambazaji wa habari za uwongo wanafurahia kuwaweka watu hofu kupitia kwa habari potovu na za uwongo. 

“Wanataka kuwapandisha watu hasira, kuwapa watu furaha, huzuni au hofu, haja yao ni kusisimua hisia za watu,” alitueleza Bwana Shiundu kwenye simu. 

Vile vile alisema watu huwa hawahakikishi kwa kuwa na haraka yakuposti kwenye mitandao na kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu. 

“Watu wengine hawana njia ya kuhakikisha jumbe zinazosambazwa na kwa sababu ya kusisimuliwa kwa hisia zao na jumbe hizo, wanasambaza.”

This is an edited and translated version of a story by Sigomba Ramadhan Omar which originally appeared on The Standard.