19th Ave New York, NY 95822, USA

Habari potovu zinazosababisha kusuasua kwa kupashwa chanjo kwa watu wenye viwango vya chini vya maisha mjini Nairobi

By Samuel Abuya| August 23, 2021

Maelezo ya Mhariri

Uhamasishaji wa uma kuchuka chanjo ni moja wapo wa jambo lenye jangamoto duniani kote. Jangamoto hii ni kubwa zaidi kwenye jamii  zilizo na viwango vya juu vya umasikini. Kulingana na data iliyotolewa kwa Mradi wa Dunia wa Data kutoka Chuo Kikuu cha Oxford; Uingereza imepeana chanjo kwa asilimia sabini ya wananchi  na Marekani imepeana takriban asilimia sitini ya wananchi, dhidi ya ugonjwa wa Corona, Covid-19. Ilihali katika nchi za Afrika, Nigeria na Kenya, ni asilimia mbili tu ya watu waliochukua chanjo huku jamii zenye viwango vya juu vya umasikini zikiweka viwango vya chini zaidi vya watu waliochukua chanjo.

Ni saa nane kamili katika mji mkuu wa Nairobi. Msimu ni wa mvua nyingi hivyo basi mawingu yametanda na muda wowote sasa mvua kubwa itanyesha. 

Najitahidi vilivyo kupishana na mkusanyiko mkubwa wa watu na piki piki, boda boda nikiwa kwenye kijiji cha Kisumu Ndogo moja wapo ya vijiji kumi na tatu vilivyo kwenye makaazi makubwa duni ya Kibera yaliyoko kilomita saba kusini magharibi kutoka mjini Nairobi. 

Hatua zakuzuia usambazaji wa ugonjwa wa Covid-19 kama usambazaji wa kijamii na uvaaji wa barakoa katu hazijazingatiwi kijijini humu. Idadi kubwa ya watu barabarani hawana barakoa na walio nazo wamezivaa na kuziweka kwenye kidevu. Idadi kubwa ya wauzaji wa chakula kando kando ya barabara iliyojaa matope wanazungumza na kuwahudumia wateja bila barakoa. 

Sehemu za kuoshea mikono zilizowekwa wakati ugonjwa ulipoanza hazina maji na hakuna anayeshughulika nazo. 

Niko njiani kwenda kukutana na kundi la vijana katika makaazi haya ambalo limekuwa likipiga vita na kutupilia mbali habari potovu kuhusu ugonjwa wa Corona na wakati ule ule limekuwa likihamasisha wakaazi kuhusu umuhimu na uhitaji wakuchukua chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona zilizo anza kupeanwa na serikali mwanzo wa mwezi wa Machi mwaka huu. Shughuli hii kama watakavyo nieleza, imekumbwa na jangamoto nyingi kwa sababu ya habari potovu ambazo zimeenezwa kwa wanakijiji huku idadi kubwa ikiziamini habari hizo na kuzifuata.  

Ninapokaribia mahali pa mkutano Diana Akinyi kiongozi wangu wa mawasiliano ambaye ni mzaliwa wa kijiji hiki, ananikaribisha. 

Kikundi hiki cha vijana saba kinanisubiri kiwanjani ambapo kuna mtazamo mzuri wa makaazi haya makubwa duni. 

Makaazi ya Kibera ni makaazi makubwa na duni zaidi nchini Kenya na ya pili yenye idadi kubwa ya wakaazi barani Afrika. Hali tunayokutana nayo ni kama ya makaazi mengine duni kwenye mji wa Nairobi; yenye viwango vya juu vya umasikini, ukosefu wa ajira unaoongezeka kila kukicha na ukosefu wa mahitaji  muhimu na ya kila siku kama maji safi ya mfereji, huduma za nafuu za kimatibabu, usafi, makaazi ya sawa na stima. 

Idadi kubwa ya wakaazi wanaosemekana kuwa takriban elfu mia mbili na hamsini wanaisha china ya kiwango kinachonakiliwa na Benki ya dunia, cha dola mbili ya Marekani hiki kikiwa kiwango cha chini zaidi ulimwenguni hali ambayo imezidishwa na ugonjwa wa Corona. Jamii hii ikiwa kati ya jamii zilizo kwenye hatari kubwa zaidi ya ugonjwa huu. 

Tukiwa kwenye wimbi la tatu kama nchi, wizara ya afya imeendelea kuhimiza uma dhidi yakupuuza hatua za kuzia uenezi wa ugonjwa huu. 

Takwimu zilizopeanwa na wizara ya afya zinaonyesha kufikia tarehe ishirni na tisa mwezi wa Aprili mwaka huu, Kenya, nchi ya watu takriban milioni harubaini na saba kulingana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Imepeana chanjo kwa watu mia nane na sabini na sita elfu mia saba na nane. Mji mkuu wa Nairobi ukiwa na idadi ya watu milioni nne nukta tatu kulingana na takwimu za sensa zilizofanyawa mwaka wa elfu mbili kumi na tisa imepeana chanjo kwa watu mia mbili na sitini na saba elfu mia nne hamsini na tatu. 

Hii ikiwa chini ya lengo lilotarajiwa na ikiwa ushahidi tosha ya kutokuaminika kwa chanjo dhidi ya ugonjwa huu, jambo ambalo vijana hawa wanajaribu kukabiliana nalo. 

“Karibu sana,” Hesbon mmoja wa wale vijana saba ananikaribisha. 

Mazungumzo yanapoendelea, mmoja wa vijana hao ananionionyesha video kwenye simu yake. Video hii ilioangaliwa na idadi kubwa ya watu mtandaoni ni ya Daktari Jack Githae iliyochapishwa wakati serikali ilipoanzisha zoezi la kupeana chanjo kwa watu wengi. 

Kwenye video hii ya dakika tatu, Daktari Githae ambaye alipata mafundisho yake nchini Kenya na Australia, na ni daktari wa dawa za kienyeji anaukumbusha uma kuhusiana na nyakati za jadi ambapo chanjo ilitumika kupunguza muongezeko wa idadi ya watu duniani. Huku akiongeza kwamba msimu huu si tofauti. 

Daktari Githae ambaye pia alitangaza kwamba anaweza kuponya ugonjwa wa Corona wakati ugonjwa huu ulipoanza, kupitia kwa dawa zake za kienyeji amekuwa daktrai kwa miaka hamsini sasa, kulingana na habari anazotoa kwa uma na wanahabari. Daktari Githae aliongeza kuwa chanjo zimetumika kueneza magonjwa kadha wa kadha aliyoyataja kwenye video hiyo ambayao bado ipo kwenye mitandao ya kijamii. 

“Hii ni moja wapo ya habari potovu tunazozipinga, “ mmoja wa vijana wale anainieleza. “Habari hii imeleta kutokuamini na kukataa kwa chanjo kwa idadi kubwa ya watu kijijini humu. Daktari Githae ni daktari mwenye umaarufu mkubwa hapa kijijini ambaye anawasiliana na wana kijiji wengi ana kwa ana. Imekuwa changamoto kubwa sana kupinga habari anazozipeana kwa uma.”

“Idadi ndogo sana ya wakaazi wa kijiji hiki, wengi wakiwa hawajasoma, wanaweza kupinga au kutia shauku wanapoelezwa ujumbe kama huu na daktari kama Daktari Githae. Aliwaeleza wasiende kupewa chanjo akisema kuwa ni chanzo cha dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio. Wakaazi wengi wamefwata maagizo haya.” 

Utafiti wa kiteknolojia mtandaoni unaonyesha kuwa Daktrai Githae amekuwa mshauri na Shirika la Afya Duniani na mkufunzi na Sekretarieti ya utajiri wa Kawaida katika mkoa wa COMESA. 

Picha ya Daktari Githae alipokuwa na mahojiano na Wanahabari. .
Picha ya Daktari Githae alipokuwa na mahojiano na Wanahabari. .

 

Nazidi kuelezwa kuwa kuna habari zaidi potovu ambazo wakaazi hapa wanaamini na kufuata. 

Idadi kubwa ya wakaazi wanasemekana kuamini kuwa vinywaji vyenye mchanganyiko vinaweza kuponya ugonjwa wa Corona. Mchanganyiko huu ukiwa wa tangawizi, limau na kitungu saumu. 

Tunapokamilisha ninachukua fursa kuzungumza na mmoja wa wauza chakula kando mwa barabara. Kwa mwangalio wangu anakaa kuwa Mama wa miaka harubaini. 

“Ningependa kujua kama umepata chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Corona…?” Nina muuliza. 

Ana nijibu kwa tabasamu, “Hiyo kitu mimi sitaki.” Na kuendelea kuchoma samaki wake kwenye mafuta ndani ya karai. “Kwanza hapa kijiji sisi hatujaona mtu amekufa juu (kwa sababu) ya Corona na pia tumesikia mambo mengi juu (kwa sababu) ya hiyo sindano, “ anaongezea. 

“Tumeambiwa kuna vile inaingililia hii mabo ya akina mama ya kila mwezi (hethi.) Tena tumesikia ziko na long term effect (athari za muda mrefu) Ananieleza Mama huyu wa watoto watatu. 

Muuzaji mwingine anayeuza kando yake, anaamua kuongezea mjadala wetu kwa kusema, “Pia hii vaccine (chanjo) wanapeana watu ilikataliwa kule majuu. Mbona gava (serikali) idunge wasee (watu) kitu ilikataliwa kwingine na tuliona. “

Katika mahojiano ya simu na Daktari wa zamu, Brian Kimani, Daktari Kimani alitueleza, “Kumekuwa na ukosefu wa mafundisho na uhamasishaji wa uma kuhusiana na Chanjo dhidid ya Ugonjwa huu.” Daktari Kimani anakubaliana na Kundi la Vijana wa Kibera, eneo la Kisumu Ndogo kwamba kuna umuhimu wa kuwahakikishia watu kuwa chanjo zinazopeanwa zimepitia majaribio ya kisayansi ya kutosha na chanjo hizo ziko salama kwa matumizi. 

Na kuhusiana na madai ya uponyaji kwa dawa za kienyeji wa Daktari Githae, Daktari Kimani anaeleza kuwa, “Madai hayo hayawezi kuhakikishwa na kwamba yanaweza kuwa ya uwongo.”

Hali inayoletwa na habari potovu kuhisana na chanjo ni ile ile katika vijiji vingine kwenye makaazi ya Kibera na vitongoji vingine vinavyofanana na makaazi hayo mjini Nairobi. Tulitembea eneo la Mathare ambalo ni la pili kubwa zaidi lenye makaazi duni ya mabanda na eneo la makaazi ya mabanda la Mukuru na tukashuhudia kuwa watu wamerejea katika hali yakawaida ya maisha. Wengi hawajapewa chanjo dhidi ya Corona na hawazingatii hatua za kupunguza uenezi wa ugonjwa huu. Idadi kubwa haiamini chanjo hizi kuwa sawa. 

Shirika la Afya la Dunia limehakikishia watu usalama na ufanisi wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Cororna, Covid-19. 

Kituo cha uzuizi na udhibiti wa magonjwa vile vile kimetoa maelekezo kuhusiana na vile chanjo hizo vinavyofanya kazi. Kulingana na kituo hiki chanjo hizo zinatusaidi kupata kinga dhidi ya virusi vinavyo sababisha Covid-19 bila ya anayepashwa chanjo kupata virusi hivyo. 

Kulingana na Wizara ya Afya nchini Kenya kumepatikana visa mia moja sabini na moja elfu na vifo elfu tatu mia mbili ishirini na tatu tangu mwanzo wa janga hili.

Serikali inatakiwa kuanza zoezi kubwa la kupeana chanjo amabalo linalenga watu million kumi kufikia mwezi wa sita mwaka ujao. Lakini ikiwa zoezi hilo litakumbwa na habari potovu na ukosefu wa uaminifu ambao umeshuhudiwa katika awamu ya kwanza ya zoezi hili. Basi serikali inapaswa kutilia mkazo kampeini za elimu kwa uma ya umuhimu na uhitaji wa kuchukua chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona, ili kupiga vita habari potovu zinazoendelea kuenezwa kuhusiana na chanjo hizo kila uchao.  

This is an edited and translated version of a story by Samuel Abuya which originally appeared on Africa Global News.