19th Ave New York, NY 95822, USA

Athari za kikweli za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19

By Cece Siago| August 23, 2021

Maelezo ya Mhariri

Watu husema, “Picha huwa haidanganyi.” Lakini video za uwongo zimekuwa chanzo kikuu cha habari potovu wakati huu wa janga la Corona. Kuna wale watapeli wanao chukua video za wanahabari na kuweka jumbe zao za uwongo huku wengine wakibadilisha sauti hivyo basi kufanya video ya mgonjwa mahututi kuwa video ya mtu anayeugua kutokana na madhara makali ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona. Video moja ambayo ina ugumu wa kuieleza inahusu sumaku: madai yake yakiwa microchip imewekwa kwenye maji na kutiwa kwenye sindano.

Kwa kifupi video hii haina ushahidi wa kisayansi na ni ya uwongo. Hatari ni kwamba athari za video hizi kama kusuasua kwa uma kwenye zoezi la kupashwa chanjo dhidi ya Corona ni kubwa. 

Wakati nchi ya Kenya inapojiandaa kwa awamu ya pili ya zoezi la kupashwa chanjo dhidi ya maradhi ya Covid-19 linalotarajiwa kuanzaa mwezi wa Juni mwaka huu, video za wanaodai kuwepo kwa athari za chanjo hizo zimeanza kuzuka na kusababisha kusuasua kwa wananchi wa kawaida. 

Video hizi ziko katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp na zinasambabzwa kwa wingi kwenye mtandao huo changamoto kwa wengi ikiwa kubainisha uhakika na usawa wa habari zilizoko kwenye video hizo. 

Jane Wanjiru alikuwa amekaa kwenye deski lake la kufanyia kazi alipopata ujumbe katika simu yake. Alifungua ujumbe huo na mara moja akamwita mfanyi kazi mwenzake na kumwonyesha ujumbe huo wa video. 

“Huu ndo ukweli haswa wa jinsi utakavyofanyika ukishapashwa chanjo,” anamueleza wanapotazama video hiyo. 

Ni video ya mwanamume anayesema yeye ni daktari na mwanasayansi anayedai kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona inasababisha kuganda kwa damu mwilini.

Wanaanza kujadiliana kuhusiana na ujumbe wa daktari huyu kabla ya Jane kumsambazia mfanyikazi mwenzake video hiyo ambayo mfinaykazi huyu ataisambaza kwa jamii na marafiki zake. 

Hivi ndivyo habari potovu; usambazaji wa habari za uwongo na zisizo na uhakika, unafanyika kati ya wakenya.

Kwenye masaa machache yajayo, Jane atakuwa amesabaza ujumbe wake kwa watu wengi walio katika orodha yake ya mawasiliano. 

Kusuasua kwa kupashwa chanjo kati ya wakenya kumezuia jitihada za kupeanwa kwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kati ya wakenya huku wengi wakihofia athari za chanjo hizo. 

Kusuasua huku kumeongezwa na usambazaji wa video zinazosemekana kuwa za wataalam au waathirika wa madhara ya chanjo hizo athari kubwa zaidi ikiwa kuganda kwa damu mwilini. 

Hii imesababisha wakenya wengi kuwa waathirika wa kuamini habari potovu zilizoko katika video hizo na kukataa kupashwa chanjo amabyo ni moja wapo ya mikakati ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Corona. 

Hata hivyo maelezo kutoka kwa waliopewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona kama AstraZeneca yanatofautiana na mengi yanayosemwa katika video hizo. 

Vyombo vya habari vya The Nation vilifanya utafiti nakugundua licha ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter kujaribu kupunguza usambazaji wa video zenye habari potovu, video hizo bado zinasmbazwa kwa wingi. 

Kwa mfano katika video ya dakika mbili inayosambazwa kwenye mtandao wa Whatsapp, Jamaa anayejitambulisha kama Daktari Sucharit Bhakdi anawashauri watu haswa watoto wasipasipewe chanjo kwani itasababisha kuganda kwa damu mwilini. 

Utafiti kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter kupitia, Advanced Search, kunaonyesha kuwa video ya daktari huyu ilichapishwa kwa mara ya kwanza tarehe 28 mwezi wa Mei mwaka huu. Katika hotuba yake anawaonya wengi dhidi ya kupashwa chanjo haswa watoto wadogo. 

Janga la Corona nchini Kenya limeonyesha urahisi wa kusambaa kwa habari potovu.

Kwa Jane, habari hizi ni za kweli na za kuaminika kwani mpaka sasa hajapewa chanjo licha ya kampeini zinazoshinikiza kupeanwa kwa chanjo haswa kwa wafanyikazi wa kila siku. 

“Siwezi kuchukua chanjo hizo kama athari zake ni kama inavyosemekana. Siwezi jua itaniathiri mimi ki vipi.” Anatueleza. 

Wakenya wengi kama Jane wamekataa kupashwa chanjo kwenye zoezi ambalo limewekwa huru. Kenya inapeana chanjo ya AstraZeneca inayotoka nchini India. 

Hivyo basi ni nini haswa madhara ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona…?

Vyombo vya habari vya Nation viliwasiliana na Edith Makungu, mwalimu wa miaka hamsini na nane kutoka mkoa wa Western nchini Kenya. Edith alidungwa sindano ya kwanza ya AstraZeneca na hivi sasa anasubiri kudungwa sindano ya pili na ya mwisho. 

“Nilipodungwa sindano nilikuwa na hofu kwa sababu ya yale niliyoyaona kwenye mtandao kuhusiana na majaribio ya chanjo hizi kama kuganda kwa damu mwilini,” anaeleza. 

Hata hivyo Edith alidungwa sindano kama walimu wenzake, walimu wakiwa kati ya waliorodeshwa kama wafanyikazi wenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu na kuusambaza kwa wanafunzi wao. 

Kwa Bi. Makungu madhara ya chanjo hii ilikuwa, kuumwa na kichwa, kupotea kwa nguvu mwilini na kichefuchefu kwa siku tatu kabla ya kupata nafuu. 

“Sikujihisi nikiwa na hali yoyote ya tofauti, hadi hapo baadaye nilipoaanza kuhisi kuchoka, nikaanza kuhisi uzito kwenye mkono wangu na nikahisi mwili wangu unahitaji kupumzishwa,” anaeleza. Huku akiongezea kwamba alihisi hali hii kwa siku mbili na baadaye akahisi kusikia nafuu.

Haya yanajiri baada ya wataalam kutupilia mbali madai kuwa kupashwa chanjo kunasababisha kuganda kwa damu mwilini. Huku wakilaumu uenezi wa habari potovu kama chanzo kikuu cha kusuasua kwa watu kupashwa chanjo dhidi ya ugonjwa huu. 

Habari potovu zinazodai kuwa hakujakuwa na majaribio ya chanjo hizi kwa wanyama zimechangia pakubwa kusuasua kwa watu dhidi ya kupashwa chanjo, lakini hakuna ukweli wowote katika habari hizo,” alisema Daktari Walter Jakob, profesa wa matibabu ya Biolojia na ya kitropiki. 

Kulingana na Daktari Jakob, kuna zaidi ya chanjo mia mbili ambazo hazitatumiwa na watu kwa sababu za kiusalama. 

Alilaumu kusuasua kwa kupashwa chanjo kwa kampeini za kukataa chanjo zinazofanywa na watu wa nchi za kigeni, akisema kuna hatari kubwa yakueneza video za habari potovu na za uwongo katika nchi zilizo na viwango vya chini vya maisha kama Kenya. 

Hata hivyo serikali imeendelea na kampeini za kuwarai watu haswa wazee kupashwa chanjo kwa kudungwa sindano ili kuzuia kuenea kwa maradhi ya Covid-19. 

This is an edited and translated version of a story by Cece Siago which originally appeared here.